Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MAJUKUMU NA KAZI ZA SEKTA YA UCHUKUZI

MAJUKUMU NA KAZI

Kulingana na Hati (Instrument) iliyotolewa na Mhe.Rais, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Uchukuzi imepewa majukumu ya kusimamia masuala yafuatayo:-

  1. Kutunga Sera zinazohusu Sekta katika masuala ya Uchukuzi na Hali ya Hewa na kusimamia utekelezaji wake.
  2. Kuratibu na kusimamia shughuli za Utoaji wa Leseni za usafirishaji.
  3. Kusimamia masuala ya Usalama wa usafiri wa Anga.
  4. Kusimamia masuala ya Usafiri na Uchukuzi wa Anga
  5. Kuendeleza na kusimamia Viwanja vya Ndege (vikubwa na vidogo) na huduma zake.
  6. Kuendeleza na kusimamia Miundombinu ya Reli na Huduma zake.
  7. Kuendeleza na kusimamia miundombinu ya Bandari na Huduma zake.
  8. Kusimamia masuala ya Ulinzi na Usalama katika Sekta ya Uchukuzi.
  9. Kuendeleza na Kusimamia miundombinu ya Hali ya Hewa na Huduma zake.
  10. Kuongeza tija (Utendaji kazi) na kuendeleza Rasilimali watu.
  11. Kusimamia Idara za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma,
  12. Programu za Miradi iliyo chini ya Wizara.