Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

UONGOZI WA BANDARI YA TANGA WAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile ameupongeza uongozi wa  Bandari ya Tanga kwa utekelezaji haraka wa maagizo yaliyotolewa na vio ngozi wa juu wa Serikali

Mhe kahenzile ameyasema hayo wakati wa muendelezo wa  ziara zake za kuzungumza na Uongozi,kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi ambapo ametembelea Bandari ya Tanga, Bandari ndogo za Pangani,Kipumbwi,Mkwaja, Ofisi za Shirika la Reli Tanzania na Uwanja wa Ndege wa Tanga Mkoani humo .

Mhe Kihenzile amesema  katika ziara yake hiyo mepata taarifa  maendeleo mbalimbali na amefurahishwa na kiwango cha utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya viongozi waqliofanya ziara kabla yake

“Nimefurahi maagizo yametekelezwa likiwemo la kuwa na Pantoni ambalo ni agizo la Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa,agizo la kufunga CCTV Camera alilolitoa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango ambapo zimefungwa camera 49 na agizo la kuhakikisha Reli inaingia Bandarini ili kurahisisha upakiaji na upakuaji wa mizigo utekelezaji wake unaendelea na kumtaka Mtendaji Mkuu wa TPA na meneja wa TRC kuhakikisha linamalizika”amesisitiza Kihenzile

Mhe Kihenzile amesema Bandari ya Tanga inaendeshwa kwa ufanisi kwani mwaka 2021/2022 walipangiwa kuhudumia mzigo wa metric tani 870,000 wao wakahudumia metric tani 987,000  hivyo mwaka huu wa fedha 2023/2024 Bandari ya Tanga imepangiwa kuhudumia Mzigo wa Metric Tani Mil 1.2 kwa sababu Taifa linategemea sana mafanikio ya bandari hii ili inufaishe wananchi

Akizungumzia Bandari ndogo za Pangani,Kipumbwi na Mkwaju amesema  Bandari za Pangani na Kipumbwi zimekuwa zikifanya vizuri ambapo zimefanikiwa kuhudumia mzigo wa zaidi ya Tani 2,500 huku Bandar ya Mkwaju ikisafirisha metric tani 33,000 za Mifugo kwa kuitambua umuhimu huo Serikali ikaamua kuzirasimisha mwaka 2022

Awali akimkaribisha Mhe Kihenzile Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Masoud Mrisha amesema Bandari ya Tanga ni miongoni mwa Bandai kuu 3za mwambao wa bahari ya Hindizilizo chini ya TPA na inasimamia Bandari 3 za Pangani,Kipumbwi na Mkwaja zinazopatikana maeneo ya Pangani na Sahare mkoani Tanga

Bw.Mrisha amesema kwa upande wa utendaji kwa miaka mitatu kuanzia Mwaka 2020 mpaka 2023 kwa Bandari ndogo za Pangani,Kipumbwi na Mkwaja ni wa kuridhisha ambapo Pangani ilihudumia Shehena zilizopanga toka  Metric Tani 13,597 mpaka 49,524,Kipumbwi 18,750 mpaka 63,414 na Mkwaja shehena 5,202 Mifugo 19,282 mpaka shehena 22,483 na Mifugo 99,063 huku zikikisanya jumla ya mapato ya Mil 804 na kwa robo ya mwaka 2022/2023 zimehudumia tani 14,953 na Mifugo 9,731 Mkwaja  na mapato Mil 22

Sambamba na kufanya Ziara Bandari ya Tanga na Bandari ndogo za Pangani, Kipumbwi na Mkwaju Mhe Kihenzile pia alitembelea Ofisi za Shirika la Reli Tanzania kanda ya Tanga na Uwanja wa ndege wa Tanga na kusema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan itafanya maboresho ambayo ni sawa na kuujenga upya uwanja wa ndege wa Tanga wenye sehemu mbili za miruko za lami na nyasi

“Serikali itafanya maboresho makubwa ambayo ni sawa na kuujenga upya uwanja huu wa ndege wa Tanga  ambapo itaongeza sehemu za miruko kutoka mita 1268 mpaka 1800 kwa lami na kutoka mita 1,400 mpaka 1,500 zilipokuwa nyasi kwenda kiwango cha changarawe, ujenzi wa termino kubwa,ofisi na mnara wa kuongozea ndege” amesisitiza Kihenzile

Ameongeza kuwa maboresho hayo yatasaidia uwanja kuhimili ndege kubwa ili kuendana na mahitaji ya sasa na kuzidi kufungua fursa zilizopo Mkoa wa Tanga