Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

SEKTA YA UJENZI YAAGIZWA KUSIMAMIA TAASISI ZAKE.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kuhakikisha inazisimamia Taasisi zake kutekeleza majukumu yao  katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, nyumba na majengo ya Serikali.

Akizungumza jijini Dodoma, katika kikao cha kupokea na kujadili kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Sekta hiyo kwa kipindi cha nusu mwaka cha Julai hadi Desemba iliyosilishwa kwa Kamati hiyo,Mwenyakiti wa Kamti hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, amesema kuwa  pamoja na mambo mengine amesisisitiza umuhimu wa Sekta hiyo kuongezewa fedha ili kutekeleza na kumaliza miradi hiyo kwa wakati.

“Niipongeze Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa miradi inayoendelea, Tumeshuhudia baadhi ya miradi kukamilika na mengine kuendelea na utekelazaji wake katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo naiomba Serikali iendelee kuitengea fedha za kutosha Sekta hii ili iendelee kutekeleza na kukamilisha miradi iliyopanga”, amesema Kakoso.

Aidha, ameiagiza Wizara kuiwezesha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuweka mpango madhubuti wa kununua vipuri vya jumla kupitia kwa Makampuni halisi ya magari badala ya kupitia kwa mawakala, hali inayopelekea kwa Wakala kushindwa kufanya matengenezo ya washitiri wake kwa wakati.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Godfrey Kasekenya, ameaiahidi Kamati hiyo kuendelea kutekeleza miradi yote kwa ufanisi kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoweka pamoja na Ilani ya CCM ya Mwaka 2020.

Kasekenya, ameongeza kuwa Wizara (Ujenzi) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha kuwa fedha za Makandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali inayotekelzwa na kusimamiwa na Sekta hiyo nchini zinalipwa kwa wakati.

Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Gairo, Mheshimiwa Ahmed Shabiby, ameupongeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kujenga na kukarabati barabara nchini ambapo ametolea mfano wa barabara ya Morogoro – Dar eneo la Gairo lililokarabatiwa hivi karibuni.