Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

NAIBU WAZIRI KIHENZILE AITAKA TRC KUONGEZA KASI KATIKA KUSIMAMIA MIRADI


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile ameutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) kuongeza kasi katika kusimamia miradi inayoendelea ili ikamilike kwa wakati na kwa thamani halisi ya fedha.

Mhe kahenzile ameyasema hayo wakati alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRC) na Kujionea   miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na  shirika Hilo katika stesheni ya Dar es salaam.

“Naupongeza uongozi wa Shirika kwa usimamizi makini wa miradi inayoendelea ya uboreshwaji wa reli ya kati na ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) ,ununuzi wa  mabehewa na vichwa vya treni, Miradi hii kwa sasa ni jicho la nchi yetu hivyo natoa rai kwenu muongeze kasi ya usimamizi ili ikamilike kwa wakati na thamani halisi ya fedha kwani tunaitegemea sana ili kuinua uchumi wa wananchi ”amesema Mhe Kihenzile

Akitoa salamu za Shirika Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bi. Amina Lumuli amesema shirika hilo  liliundwa mwaka 2017 baada ya kuvunjika kwa RAHCO na TRL  na kurithi majukumu  yaliyokuwa yakitekelezwa na mashirika hayo ikiwemo kuanzisha,kusimamia,kuendeleza miundombinu ya Reli, kutoa huduma,kufanya ukarabati,kuingia mikataba na kuimarisha vitendea kazi kulingana na sheria ya reli namba kumi ya Mwaka 2017.

Aidha, Bi Amina ameongeza kwa kusema kuwa Shirika lilipata mkopo  wa Dola za  Kimarekani  Milioni 300 kutoka Benki ya Dunia mwezi machi,2014 kwa ajili ya kuendeleza  na kuboresha mradi wa usafirishaji wa reli  kutoka tani 135 km ekseli hadi tani 18.5, uboreshaji madaraja na ununuzi wa mabehewa 44 ya mizigo ambavyo vimeshakamilika.

Kwa upande wa Reli ya Mwendokasi(SGR) Bi Amina amesema ujenzi wa reli kutoka DSM hadi Mwanza wenye jumla ya km 1,596 unaohusisha km 1,219 njia kuu na km 377 za mapishano umefikia katika hatua mbalimbali za utekelezwaji  zilizogawanywa kwa vipande vitano kwa awamu ya kwanza  ambavyo ni Dsm-Moro(km300) asilimia 98.52, Moro-Makutupora(km422) asilimia 94.99, Makutupora-Tabora(km368) asilimia 10.92, Tabora-Isaka(km 165) asilimia 4.63 na Isaka-Mwanza (km 341) asilimia 37.22.

Ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea vizuri awamu ya kwanza na kwa awamu ya pili ya kipande cha Tabora-kigoma(km 506) usanifu unaendelea ambapo mpaka sasa jumla ya Dola za kimarekani Bil 3.75 sawa na Zaidi ya shilingi tril 23 zimeshatumika na tayari jumla ya vichwa vya treni vya umeme 17 na seti 10 za EMU ukarabati unaendelea Nchini korea,mabehewa ya mizigo 1,430 yameagizwa na tayari mabehewa ya abiria 59 yalishawasili.