Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YA ANGA NCHINI


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na mamlaka za usafiri wa anga Nchini ikiwemo zile za udhibiti, Uangalizi, Watumiaji na Waandaaji wa miundombinu ya usafiri wa Anga  Nchini licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali

Ameyasema hayo , Mhe kakoso wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Serikali iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo taasisi za TCAA, TAA, ATCL na KADCO ziliielezea  kamati utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa  kisekta na maendeleo ya sekta ya usafirishaji kwa njia ya anga nchini

“kamati imesikia mipango ya sasa ,baadae na kujionea hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa faida ya sekta ya usafirishaji kwa njia ya Anga nchini kama vile ufungaji wa rada mpya nne, maeneo ya Dar es salaam, Kilimanjaro ,Mwanza  na Songwe, ufungaji wa mtambo mkubwa wa kuwezesha ndege kutua kwa usalama, Maboresho ya uendeshaji kibiashara kwenye viwanja vya ndege na ongezeko la safari za ndege Nchini.’ amesisitiza Mhe Kakoso

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya maboresho ya sekta ya anga nchini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini, ununuzi wa rad na ndege mpya.

Aidha, Waziri Mbarawa ameongeza kwa kusema kuwa,  Serikali ya Awamu ya sita kupitia, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa zile taasisi ambazo zina uwezo wa kuzalisha na kuajiri ziajiri moja kwa moja hivyo utaratibu mzuri utakuja na changamoto hii itapungua  kwenye taasisi zote.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Ndugu Daniel Malanga ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi na maboresho ya miundombinu mbalimbali kwa mustakabali wa maendeleo ya usafiri na Usafirishaji kwa njia ya Anga nchini,

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inaendelea na ziara zake za kutembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni maandalizi ya  Mkutano wa kumi na moja wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 04 April,2023.