Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), (hawapo pichani), wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja hao na Waziri huyo jijini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge wakiwapongeza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na Manaibu wake Eng. Godfrey Kasekenya na Atupele Mwakibete mara baada ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/24 kupitishwa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Gabriel Migire (wa pili kulia) pamoja na uongozi na watumishi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo bungeni jijini Dodoma, tarehe 22 Mei, 2023.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Profesa Makame Mbarawa, akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma leo Tarehe 22 Mei, 2023
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila pamoja na Mwakilishi wa kampuni ya Mkandarasi JIANGXI GEO-ENGINEERING GROUP Limited kutoka China wakionesha mikataba ya mradi wa Ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom km 25, Mkoani Manyara.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya (wapili kulia), na viongozi wengine alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mianzini-Ngaramtoni juu KM 18 wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya (wapili kulia), na viongozi wengine alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mianzini-Ngaramtoni juu KM 18 wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu - Loliondo sehemu ya Waso –Sale (KM 49) wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo mkoani humo.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa barabara ya Mto wa Mbu - Loliondo sehemu ya Waso –Sale (KM 49) wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila na Mwakilishi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. (CHICO), wakisaini mikataba ya mradi wa ujenzi wa Barabara za Maingilio katika Daraja la Sibiti, Noranga-Doroto na Itigi-Mkiwa, Mkoani Singida.
Hatua iliyofikiwa ya Ujenzi wa jengo la Zimamoto katika Kiwanja cha Ndege cha Musoma
Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Balozi, Eng. Aisha Amour akiendesha gari lililobuniwa na kampuni ya KAPEE Motors linalotumia umeme ambalo ni sehemu ya bunifu za watanzania katika Mkutano mkuu wa tano wa Mafundi Sanifu unaoendelea jijini Mwanza.
Kazi zikiendelea za ujenzi wa moja ya makalvati katika barabara ya Ntendo – Kizungu (km 25) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Rukwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akisaini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga na Mwakilishi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China kwa gharama ya Bilioni 55.908 kwa muda wa miezi 18, mkoani Rukwa.
Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi) wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi 2023 yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi) wakipita mbele ya Mgeni Rasmi, katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi 2023 yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire, katika picha ya pamoja na Wanamichezo wa Uchukuzi SC , wakati alipowatembelea mkoani Morogoro. Wanamichezo hao wanashiriki katika mashindano ya Mei Mosi ambayo kwa mwaka huu yanafanyika Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini-Uchukuzi, Bi Devota Gabriel akifungua kikao kazi cha kufanya tathmini ya mikataba ya utendaji kazi kwa kipindi cha nusu mwaka 2022/2023 kati ya Wizara na baadhi ya Wakuu na Wawakilishi wa Taasisi 14 zilizo chini ya Sekta hiyo,kilichofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jakaya Kikwete , Jijini Dodoma.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Barabara ya Kazilambwa hadi Chagu (KM 36) inayojengwa kwa kiwango cha Lami, Mkoani Tabora. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2023
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Sekta hiyo, mara baada ya kufungua baraza la Sekta ya Ujenzi, Jijini Dodoma.
Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu ambalo ni sehemu ya barabara ya Kidatu hadi Ifakara (km 66.9) inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Morogoro ambao ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 78 na unagharimu kiasi cha Bil 105.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa azungumza na wadau wa Uchukuzi katika mkutano maalum ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Biashara jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka BRT, Eng. Barakaeli Mmari alipokagua Mradi wa BRT III, kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto ambao ujenzi wake unaendelea.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete na Mshauri wa Waziri kutoka Ubalozi wa China Nchini, Suo Peng wakiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya Wahandisi na watendaji waliofariki katika ujenzi wa reli ya Shirika la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Tanga, mwishoni mwa wiki.
Title | Tarehe | Pakua |
---|---|---|
TANGAZO LA KOZI MAALUM YA MAOPARETA WA MITAMBO YA KAZI ZA UJENZI (GRADER OPERATOR COURSE) | 2022-11-09 | Pakua |