Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi anayesimamia mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato, Ayele Yirgo, wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Mhandisi Aisha Amour akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Njombe wakati alipotembelea Barabara ya Makete-Isyonje inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha Lami, Mkoani humo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Barabara sehemu ya Barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta Ujenzi), Mhandisi Light Chobya, akizungumza na watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe (hawapo pichani).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Mhandisi Aisha Amour, akizungumza na watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe (hawapo pichani), wakati walipofanya kikao kazi na watumishi hao kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi.
Muonekano wa Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), ambao ujenzi wake kwa njia nane ukiwa unaendelea jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Sekta ya Uchukuzi, Bakari Mtila akitoa elimu kwa mmoja wa watoto waliotembelea banda la Sekta hiyo katika maonesho ya nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Barbara ya Kikusya-Ipinda- Matema KM 39 Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu akisogeza kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa kituo cha forodha cha pamoja Kasumulu Wilayani Kyela (mpakani) na Malawi Mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Barabara ya Chunya-Makongorosi (KM 39) iliyojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Chunya-Makongorosi (KM 39) iliyojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete (wa sita kushoto) katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Boeing Afrika, mara baada ya kufungua mkutano wa siku moja wa shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi zawadi Waziri Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailogly mara baada ya mazungumzo yao mjini Ankara Uturuki
Muonekano wa Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) ambayo imefunguliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Baadhi ya watumishi wa Sekta ya Ujenzi na Taasisi zake wakifanya mazoezi wakati wa Bonanza katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo za kusanifu na kujenga barabara na madaraja kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini (waliosimama), kwenye warsha ya kujadili namna ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye miundombinu ya barabara, iliyoandaliwa na Bodi ya Mfuko wa Barabara jijini Mwanza
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Dk. Ombeni Swai mara baada ya kuizindua Bodi hiyo, katikati ni Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro akishuhudia.